kufuatia matamshi aliyotoa kuhusu mchezaji mwenza Steph Curry.

Nyota wa mchezo wa mpira wa vikapu nchini Marekani LeBron James amemuita rais wa Marekani ‘Bum'{Makalio} kufuatia matamshi aliyotoa kuhusu mchezaji mwenza Steph Curry.

Trump alisema kuwa klabu ya Golden State Worriers haitaruhusiwa kuingia katika ikulu ya Whitehouse baada ya nyota Curry mwenye umri wa miaka 29 kusema kuwa hataki kwenda Ikulu hiyo.

”Kwenda ikulu ya Whitehouse ilikuwa heshima kubwa hadi ulipoingia katika jumba hilo”, alisema James mwenye umri wa miaka 32.

Siku ya Ijumaa Trump alisema kuwa wachezaji wa NFL waliofanya mgomo wakati wa nyimbo ya taifa wanafaa kufutwa kazi.

Washindi wa mchezo wa vikapu nchini Marekani Golden State Warriors kutoka Florida walikuwa wanapanga kukataa mwaliko wa kawaida wa kusherehekea ushindi wao katika ikuku ya Whitehouse.

Curry anasema kuwa timu hiyo inaweza kushinikiza mabadiliko katika ikulu hiyo iwapo itakataa mwaliko .

”Sitaki kwenda Ikulu kwa sababu itaonyesha kuwa wachezaji hawajui vitu ambavyo amekuwa akisema na vitu ambavyo hakusema kwa nia nzuri.

Aliongezea: Sidhani kwamba kwa sisi kwenda katika Ikulu ya Whitehouse kutaimarisha mambo, na hii ni fursa yangu kusema.

Lakini Trump alijibu kwamba mwaliko huo umefutiliwa mbali.

story@moodyhamza