Juma Nature Anasema Siwezi Kuacha.


Msanii Juma Nature ambaye ni mkongwe kwenye game ya bongo fleva Juma Kassin Nature, amesema wasanii wanaotangaza kuacha muziki na kuendelea kuwepo wanatafuta huruma ya mashabiki, au wanawapima watapokeaje.

Juma Nature ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Television, na kusema kwamba ni vigumu kwa mwanamuziki kuacha kufanya muziki, hivyo wasidanganye watu na kutafuta kiki kwa kujaribu kuacha muziki.

Source: Udaku.