Jacqueline Wolper amuumiza roho Sarah.

 

Jacqueline Wolper ametuma mashambulizi kwa mwanamke aliyemkwapua Raaj wake  Sarah. Baada ya raia huyo wa Italia kumlipua Wolper kwa kupost screeshot ya chat ya Whatsapp kwenye Instagram akimchimba mkwara, staa huyo wa filamu amejibu mapigo kwwa kupost video akiusifia wimbo mpya wa Harmonize, Shulala na kuweka kijembe.

Kwenye post moja Wolper ameandika: Haka ka nyimbo kazuriii sana na video pia ndo usiseme!..bwana Raaaaaj umejua kunyoosha!Kama bado haujaangalia video ya haka ka wimbo pita kwenye bio ya @harmonize_tz
#Uliyemchokozakaja #Shulala.. #NaUkinibipuTuNakupigia.”

Na nyingine ameandika: Shulala ni fire 👌 #uliyemchokozakaja

#Uliyemchokozakaja #NaUkinibipuTuNakupigia.”

Wolper na Harmonize waliachana miezi kadhaa iliyopita na kila mmoja akashika njia yake. Harmo alizama kwa mzungu wake Sarah na Wolper kupata huba toka kwa BFF wake, Brown ambaye hata hivyo kuna dalili kuwa hawapo pamoja tena.

Source: Dizzim Online.