Msanii wa muziki, Hussein Machozi, amefunguka kwa kudai kuwa hakuna msanii wa muziki kutoka Tanzania ambaye anajulikana nchini Italy.
Aidha amedai muimbaji kutoka Kenya, Stella Mwangi ambaye anaishi nchini Norway ndiye msanii wa Afrika Mashariki anayefanya vizuri.
Muimbaji huyo aliyewasili nchini Tanzania wiki hii akitokea Italy, amedai nchini Italy muziki wa Tanzania haujafika na hata wasanii wanaofanya vizuri nchini kwa sasa akiwemo Diamond na Alikiba hawajulikani.
“Hapana lakini kuna mtu mmoja alishaniambia kuhusu msanii wa Kenya anaitwa Stella Mwangi wanamfahamu fahamu, siyo kivile sana kutoka East Africa,” alisema Hussein.
Aliongeza, “Bongo Fleva Italy sijawahi kuisikia kiukweli wa Mungu. Kama kuna mshikaji mmoja nilimwambia kwetu kuna msanii mkali sana anaitwa Diamond nikawa nimempa link akawa shabiki, akawapa na wengine wakawa mashabiki wa Diamond kinyama.,”
Muimbaji huyo amedai amekuja nchini kwaajili ya kuachia kazi zake mpya za muziki na baada ya hapo atarejea tena Italy kwaajili ya kuendelea na masomo
Source: Udaku