Hamisa Mobeto Atishiwa.


Sakata la modo ‘grade one’ Bongo, Hamisa Hassan ‘Mobeto’ kudaiwa kuzaa kwa siri na msanii wa Bongo Fleva, limechukua sura mpya baada ya mrembo huyo kufichua kuwa anatishiwa kuuawa wakati wowote yeye na mwanaye wa kiume aliyemzaa Agosti 8, mwaka huu na kumpa jina la Abdul Naseeb a.k.a Prince Dully D’.

TUJIUNGE MBEZI-BEACH
Kwa mujibu wa chanzo makini ndani ya familia ya Hamisa yenye maskani yake Mbezi- Beach jijini Dar anakoishi mrembo huyo, baada ya kujifungua, kumekuwa na sarakasi nyingi zinazoendelea juu ya mwanaye huyo.

TIRIRIKA NA CHANZO
“Unajua baada tu ya kujifungua kulienea habari nyingi kuwa mtoto huyo ni wa msanii huyo hasa baada ya Hamisa kumpa mwanaye jina hilo.

“Kilichofuata, kwanza msanii huyo alikimbilia kwenye media (vyombo cha habari) kukanusha habari hizo ambazo zimekuwa zikizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu.
“Unajua jamaa (msanii huyo) alidhani kuna siri chini ya jua kuwa anaweza kuficha jambo hilo maana watu walikuwa wakimchomea kwa mpenzi wake ambaye amezaa naye.

HAMISA SIYO WA MCHEZOMCHEZO
“Ili kumziba mdomo Hamisa, msanii huyo aliona ni bora amkane mapema lakini Hamisa siyo wa mchezomchezo maana aligoma kuficha ishu hiyo.
“Baada ya kuona anaweza akabumburua ishu, msanii huyo alimpiga biti asizungumze na vyombo vya habari kabla ya kumwekea ulinzi wa chinichini kuhakikisha waandishi hawamfikii Hamisa.
“Sehemu pekee ambayo Hamisa aliona jamaa huyo hawezi kumzuia ni kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii hasa Instagram na Snapchat ‘so’ akawa anaposti vipande vya baadhi ya viungo vya mtoto huyo.
“Sasa baada ya kuona hivyo, msanii huyo ambaye alikwenda mara moja tu kumuona mtoto huyo alianza kumpigia simu na kumtumia meseji za vitisho.

HAMISA AISHI KWA HOFU
“Wewe fikiria Hamisa na kichanga chake sasa anaishi kwa hofu maana jamaa amemuambia kama atafunguka kuwa amezaa naye atamuondoa uhai yeye na mtoto wake.
“ Hali hiyo imeifanya family ya Mobeto iwe na hofu kubwa na ili kujiweka salama, aliona ni bora aende polisi kuripoti ili kama kutakuwa na jambo lolote baya litakalomkuta yeye na mwanaye, basi mhusika atakuwa ni msanii huyo.
“Mwanzoni tulidhani ni ishu ndogo lakini kwa vitisho anavyopokea Hamisa, vinamnyima raha na kumfanya alie tu.
HAMISA ATIA HURUMA

“Kiukweli Hamisa anatia huruma sana na anahitaji msaada kwa sababu mbali na msanii huyo pia anapata vitisho kutoka kwa mpenzi wa jamaa huyo.
“Sasa watu wanajiuliza, wakati anatembea naye hakujua kuwa kinaweza kupatikana kiumbe? Na kwa ustaa wake anashindwa nini kulihendo suala hilo kwa busara ili lisimchafulie kuliko kutoa vitisho hivyo?” kilifunguka chanzo chetu hicho na kuongeza:
“Hata kwenye ukurasa wake wa Snapchat, Hamisa ameshatahadharisha juu ya kutishiwa kuuawa yeye na mwanaye.”
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Ijumaa liliperuzi kwenye ukurasa wake huo na kukutana na ujumbe wa Hamisa uliosomeka:
“Mlidhani atafia tumboni enh…au mlijua nitafia leba…. nyie siyo Mungu na hamtakaa kuwa kamwe…& if anything bad and I mean anything bad happens to me or my son hatutawaacha salama!!!”

HUYU HAPA HAMISA
Kufuatia hali kuwa tete huku Hamisa akidaiwa kuwa kwenye msongo, Ijumaa lilimtafuta staa huyo ambapo kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalum alikiri kupokea vitisho kutoka kwa msanii huyo na kwamba ameamua kutokaa kimya na badala yake kwenda kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ikiwemo kwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI).
‘MIMI NA MWANANGU TUNAUAWA WAKATI WOWOTE’
“Ni kweli mimi na mwanangu tunauawa muda wowote. Nina ushahidi wa kutosha wa vitisho so nimeona ni vyema nitoe taarifa kwenye vyombo vya usalama,” alisema Hamisa kwa kifupi na kuahidi kulifungukia suala hilo kwa kirefu zaidi muda si mrefu.
TUMEFIKAJI HAPA?

Tetesi za Hamisa ambaye ni mwanamitindo wa kitaifa na kimataifa na video queen matata kutoka na msanii huyo zilianza baada ya kufanya naye kazi katika ‘project’ ya wimbo.
Mara baada ya kujifungua, mama na dada wa msanii huyo walikwenda hospitalini kumjulia hali Hamisa, jambo ambalo lilisherehesha sakata hilo kuwa mtoto huyo ni damu yao.
Awali mrembo huyo ambaye kabla ya sakata hilo alizaa mtoto wa kike na bosi wa redio, alimfungulia mwanaye huyo akaunti ya Instagram kwa jina ‘Tanzania Baby’, lakini baadaye aliibadilisha na kuiita Abdul Naseeb_tz ambayo kwa sasa ina wafuasi zaidi ya laki moja.

Source: Udaku