Msanii Gigy Money amewausia wasichana ambao wameingia kwenye ‘game’ ya bongo fleva na kuwataka waache kuimba vitu vigumu na badala yake watafute vyepesi ili waweze kuwafikia mashabiki zao kwa wepesi kama alivyofanya yeye.
Gigy Money amesema hayo baada ya kuwepo wimbi kubwa la wasanii wapya wakijikuta kutumia vitu vingi katika kuimba na mwishowe kutofikisha malengo yao waliyoyaweka kwa wakati huo.
“Nitoe ushauri kwa wasichana ambao wanaimba, unajua wasichana wengi wana vipaji vya kuimba lakini wanafeli. Ukishajijua huwezi kuimba acha kuimba vitu vingi, huna uwezo wa kuimba alafu mambo unayoimba mlolongo kibao, vingereza, sijui nini utajikuta unafeli. Sasa neno kama ‘papa’ lipo uswahilini, rahisi kwa watu kuelewa”, amesema Gigy Money.
Hivi karibuni Gigy Money ameachia wimbo wake wa ‘papa’ ambao unazidi kufanya vizuri mtaani, na kusema kwamba lengo lake lilikuwa kuwafikia watu wa rika lote, na anahisi amefanikiwa katika hilo.
Source: Udaku.