G.Nako Hakunishawishi Asema Rapper ZaiiD.

Rapper wa SSK, ZaiiD amesema si kweli kwamba style ya G Nako ya kuimba na kurap katika game ilimshawishi kufanya ngoma yake ‘Umeme Umerudi’.

ZaiiD amesema [sociallocker id=5327]chimbuko la ngoma hiyo ni kutokana na yeye kusikiliza aina nyingi za miziki tofauti lakini anaheshimu anachofanya G Nako katika game ya Bongo Flava.

“Hapana, mimi pia ni shabiki wa aina nyingi za rap, sijui kwa sababu G Nako naye amefanya, Ngwea alikuwa anaimba na kuchana, Chidi Benz hivyo hivyo, mimi nilikuwa nikisikiza miziki mingi sana” ZaiiD.

“Namuheshimu G Nako kwa anachofaya ila hakuni-inspire kufanya umeme, niliamua kwa sababu nilihisi ni muda halisi wa kuongea vitu ambavyo vitasika mwanzo hadi mwisho kwa ukaribu na urahisi” ameongeza.

ZaiiD kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Wowowo’ pamoja na ile ya kundi (SSK), Slow Down.

Source: Bongo5 [/sociallocker]