Faida za Kunywa Mji Katika Mwili wa Binadamu

Hizi Hapa Faida za Kunywa Maji Katika Mwili wa Binadamu

 

Kunywa maji ni tendo ambalo watu wengi hulifanya pale wanapohisi kiu. Wengine hutumia vinywaji mbalimbali kama vile juisi au soda ili kutuliza kiu. Wataalamu wanashauri matumizi ya maji kwa kutuliza kiu na hata kwa kunywa polepole kwa lengo la kuufanya mwili usikose maji.

Kwa nini maji? Je, yana umuhimu gani katika mwili.

Umuhimu huo ni miongoni mwa mambo yaliyotiliwa mkazo na madaktari wa binadamu wakati walipokutana na wagonjwa mbalimbali wenye magonjwa sugu.

Mtaalamu wa Magonjwa ya Moyo, wanaelelezea umuhimu wa maji ya kunywa ili kuepuka magonjwa ya moyo.

“Moyo hauwezi kufanya kazi bila maji ambayo ni asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kwa hiyo, unywaji wa maji ni muhimu kwa utendaji wa mwili na hasa zaidi kwa mishipa ya moyo,”

“Nini kinatokea kama mtu hatakunywa maji?
Kwanza, mishipa midogo ya damu katika mwili itafunga. Hii itasababisha upinzani katika mzunguko wa damu na kusababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu. Ukosefu wa maji huongeza hatari kwa moyo.”

“Kutumia glasi tano za maji au zaidi kwa siku kwa kiasi kikubwa hupunguza mashambulizi ya moyo kwa kiasi kikubwa, ikilinganishwa na kunywa chini ya glasi mbili za maji kwa siku.”

Zipo faida nyingi za matumizi ya maji iwapo yatatumika kwa kiwango kinachotosheleza. Maji hufanya damu kuwa nyepesi kama inavyotakiwa kuwa, hurahisisha mzunguko wa damu kwenda kwenye moyo, hufanya moyo kutumia nguvu kidogo kusukuma damu na hata kupunguza hatari ya damu kuganda.

Wataalamu wanashauri matumizi ya kubadili tabia kama sehemu ya kukabiliana na maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufuata ushauri wa kitaalamu.

@moodyhamza