Dogo Janja afungua kwa nguvu mlango wa Suprise Music.

Msanii wa muziki wa kizaki kipya na Staa wa ngoma ya ‘Ukivaaje Unapendeza’ Dogo Janja anayefanya kazi chini ya Tip Top Connection, ameonekana kuibariki studio mpya inayohusika msanii Ray Vanny ‘Suprise Music’ kwa kuachia wimbo mpya uliyotayarishwa na Produza ‘Rash Don’.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Dogo Janja ameonesha dalili za kuwa wimbo huo utakwenda kwa jina la moja ya kata anayotokea iliyoko Arusha ‘Ngarenaro’ huku caption yake ikibainisha kuwa wimbo ni wenye kuzungumzi hatua ya kimahusiano kati ya mtu na mpenzi wake ya kumpekeleka nyumbani na unaweza kutajwa kuwa ni wimbo kutoka kwa msanii aliyeko ‘Main Stream’ kutoka katika studio za Suprise Music tangu studio hizo kuanza kuonekana kwa inatembelewa na wasanii tofauti wa muziki.

Mbali na Dogo Janja kuonekana kuwa tayari amekamilisha wimbo huo kutoka katika studio hizo, wasanii wengine ambao wameshaonekana kufanya kazi hapo ni pamoja na Morombosso ‘Mbosso’, Saida Karoli na wengine ambao hawaweka wazi.

Source: DizzimOnline.

 

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!