Dereva Aliyesababisha Ajali Akamatwa.


Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia dereva wa basi lenye namba za usajili T 438 ADR Charles Diamond, kwa kusababisha ajali iliyopoteza uhai wa watu mkoani Morogoro na kusababisha majeraha kwa baadhi ya watu.

 

Akitoa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Kamanda wa Polisi mkoani humo Urlich Matei, amesema mpaka sasa idadi kamili ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo ni watu watatu, ambapo wawili ni wanawake na mmoja ni mwanaume, huku mmoja wao akiwa ni mwanafunzi.

Majeruhi wa ajali hiyo ni 27 ambao wamepelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, lakini suala la utambuzi wa miili ya marehemu bado halijafanyika mpaka pale uchunguzi utakapofanyika.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi iliyohusisha gari aina ya daladala ikielekea Mvumi kugonga treni iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, kulikopelekea kuburuzwa kwa gari hiyo na kusababisha vifo.

Source: Udaku.