Blac Chyna aishitaki familia ya Kardashian.

Blac Chyna anaishtaki familia ya Kardashian. Mrembo huyo anadai kuwa familia hiyo imetumia nguvu yake kukishawishi kituo cha E! kuifuta show yake, Rob & Chyna.

Madai hayo hata hivyo yamepingwa na E! ambayo inadai kuwa ilishindwa kushoot msimu wa pili wa show hiyo sababu Chyna alikataa kukaa chumba kimoja na Rob. Pia E! haikufurahishwa na jinsi msimu wa kwanza ulivyopokelewa.

Pia Chyna anamshtaki Rob kwa kumpiga mwezi May pamoja na madai kuwa Rob alimtumia ujumbe akimtishia kujiua.

Ujumbe mmoja unasomeka, “I’m literally on the verge of killing myself and u couldn’t care less,” na “I will kill myself just to show U how serious I was about u and all this.”

Pia Chyna amesema Rob alimtumia picha za vidonge ambavyo angekunywa ili kujiua kama asingemjibu jumbe zake. Rob na Chyna wana mtoto wa kike aitwaye Dream Renée Kardashian.

Source: Dizzim Online.