AyoTV VIDEO: ‘Wasanii tumechoka ahadi sasa Dr Mwakyembe tunataka mabadiliko’- Mwakifwamba

Baada ya taarifa ya IKULU iliyoeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kuvuliwa uwaziri, sasa leo March 24, 2017 Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba amezungumzia mambo yaliyofanywa na Nape Nnauye huku akimtaka Waziri Dr Mwakyembe alieteuliwa katika wizara hiyo kufanya mabadiliko.

Akizungumza kwenye Ayo TV & millardayo.com aliyaongea haya…>>>>”Mara ya mwisho kukutana na Nape Nnauye kwenye maadhimisho ya wiki ya filamu za China tulikuwa na Naibu Waziri kutoka China. Sasa nimekuja kupata taarifa za kuwa Nape Nnauye kuwa ameondolewa na badala yake amepewa Dr Mwakyembe.

“Kiukweli tulimzoea na kuna mambo mengi amefanya lakini pia siwezi kumzungumzia sana Waziri mpya Dr Mwakyembe kwa sababu ndio kwanza ameteuliwa kuwa Waziri wa Wizara hiyo. Tunatarajia au matumaini yetu sisi atafanya kazi ataleta mabadiliko.

“Kikubwa sisi tumempokea na pia tunaomba akutane na sisi wadau wa filamu tumueleze changamoto zinazotukabili, wasanii tumechoka ahadi sasa Dr Mwakyembe tunataka mabadiliko kwenye sekta ya filamu.” – Simon Mwakifwamba.

Source: Millard ayo