ARUMUN


ARUSHA URBAN MUSIC NETWORK (ARUMUN)
Imesajiliwa kwa mujibu wa sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 ya Jahuhuri ya Muungano wa Tanzania yaani, “Sheria ya Sanaa za Taifa” (National Arts Act) na kupewa cheti cha usajili wa kuendesha shughuli za sanaa NAMBA BST/0854.
Tazama Orodha ya Wanamtandao
HAPA
Anuani kamili: S.L.P 14714
Arusha Tanzania
Simu:+255 758 276 226
au +255 765 022 224
Barua pepe:arumuntz@gmail.com


Pakua Katiba ya ARUMUN
HAPA
VIGEZO VYA MSANII KUJIUNGA ARUMUN:
Awe mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18, mwenye akili timamu.
Awe msanii mwenye shughuli na makazi ya muda mrefu zaidi katika mwaka ndani ya mkoa wa Arusha.
Awe msanii hai anayetoa kazi za sanaa mara kwa mara zenye viwango vya ubora kutoka studio zinazotambuliwa na kamati ya utendaji.


FAIDA ZA KUWA MWANAMTANDAO:
Kusajiliwa BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Kwa punguzo maalum elekezi kwa mtandao wa ARUMUN kutoka Baraza na ofisi ya Afisa Utamaduni Mkoa.Mfano; msanii binafsi badala ya kutozwa gharama halisi ya Elfu 40 BASATA, akijiunga na kuwa mwanamtandao ataweza kusajiliwa BASATA wa elfu 25 kupitia mtandao wa ARUMUN.
Kutambulika kisheria katika ngazi ya taifa kwa kupewa kibali pamoja na cheti kutoka Baraza la Sanaa Tanzania bila kusahau kitambulisho cha mwanamtandao wa ARUMUN.
Kusambaziwa taarifa na matangazo ya kazi ya sanaa katika tovuti ya mtandao na kurasa za kijamii pamoja na vyombo vya habari vyenye ushirikiano na mtandao wa ARUMUN.
Kupata elimu na ujuzi kupitia warsha zitakazoandaliwa na mtandao kwa kuhusisha wakufunzi mahiri na wataalam wa sanaa na biashara kutoka nyanja mbali mbali kila pembe ya dunia kwa hisani ya mtandao wa ARUMUN.
Kushiriki katika jukwaa za sanaa ikiwemo mashindano na matamasha ya muziki hivyo kukuza wigo wa mashabiki na hata kujiongezea thamani katika biashara ya muziki kwa hisani ya mtandao wa ARUMUN.
Kupata ofa maalum la punguzo la bei katika studio mbalimbali za kurekodi muziki na picha/filamu zenye makubaliano na mtandao wa ARUMUN.


MADHUMUNI NA MALENGO YA ARUMUN: Kujenga umoja, kuhimiza ushirikiano na kuchochea ushindani wa kimaendeleo katika kazi na maisha kwa wasanii, watayarishaji na wadau mbalimbali wa muziki mkoani Arusha na vile vile kutoa fursa za ajira kwa watanzania kupitia shughuli za uendeshaji wa ARUMUN
Kuhimiza na kuwawezesha wasanii kaskazini kujisajili Baraza La Sanaa Tanzania kwa wepesi kupitia Gharama elekezi toka BASATA kwa ARUMUN
Kuandaa mapendekezo ya udhamini na pia barua za maombi ya ufadhili katika miradi, mashindano, matamasha na warsha zitakazowajengea wasanii uwezo wa kujiongezea kipato kupitia biashara mbalimbali hususan muziki na shughuli za kiuchumi za ARUMUN


Kuhimiza na kuwawezesha wasanii kaskazini kujisajili Baraza La Sanaa Tanzania kwa wepesi kupitia Gharama elekezi toka BASATA kwa ARUMUN
Kuandaa mapendekezo ya udhamini na pia barua za maombi ya ufadhili katika miradi, mashindano, matamasha na warsha zitakazowajengea wasanii uwezo wa kujiongezea kipato kupitia biashara mbalimbali hususan muziki na shughuli za kiuchumi za ARUMUN

Kushiriki katika miradi, makongamano, mashindano, matamasha na warsha zitakazowajengea wasanii uwezo wa kujiongezea kipato kupitia biashara mbalimbali hususan muziki na hatimae kuitangaza nchi kupitia ARUMUN.
Kuwahimiza wadau na wadhamini kuitangaza sanaa ya muziki wa kaskazini na kupewa kipaumbele ili kuenea ndani na nje ya Tanzania kwa mazungumzo na makubaliano na pia kusambaza kazi/taarifa ya kazi za muziki kupitia tovuti ya ARUMUN, kurasa za mitandao ya kijamii, pamoja na vyombo vya habari vyenye mahusiano mazuri na ARUMUN.
Kuwa chombo cha kusimamia na kuhamasisha sanaa ya Muziki inayozingatia Maadili ya Taifa Mkoani Arusha ili kuchangia ufanisi wa ofisi ya Utamaduni Wilaya/Mkoa na BASATA. 
Jamii ya Mkoa wa Arusha kushirikiana/kuwasaidia Wasanii walio wanamtandao katika shughuli za muziki katika hatua mbali mbali ikiwemo utayarishaji wa kazi na pia mauzo/manunuzi ya bidhaa zitokanazo na Sanaa Ya Muziki. 
Kuwa chanzo Mojawapo cha Ripoti/Taarifa za usajili/takwimu za biashara za Sanaa ya Muziki/Wasanii wa Muziki Mkoa Arusha kwenda ofisi ya Utamaduni Wilaya/Mkoa na pia BASATA.


UTARATIBU

  • Shughuli hii ni ya watu binafsi hivyo wanamtandao wake watakuwa ni waasisi pamoja na wanamtandao wa kujiunga kwa kiingilio na ada.
  • Mwanamtandao atapewa kitambulisho baada ya kulipa ada ya ELFU KUMI itakayolipwa mara moja kwa maisha, (Au endapo mwanamtandao atakuwa amepoteza kitambulisho au kuomba kujiunga upya)
  • Mwanamtandao atalipa Kiingilo cha ELFU KUMI kila mwaka (Mwisho wa kulipa ada ya mwaka ni kabla ya mwisho wa mwezi APRILI. Katiba inaruhusu kuhaririwa kwa viwango vya ada na viingilio kulingana na kitakachoamuliwa kwa muda utakaopangwa na uongozi wa ARUMUN