Alikiba ni mwanangu wa dhahabu.

Meneja Mkubwa Fella ambaye pia ni mingoni mwa wale wanaomsimamia Diamond Platnumz amesema hilo haliwezi kumzuia kufanya kazi na Alikiba.

Kutokana na ukaribu wake na Diamond mashabiki wengi wamekuwa wakidhani kuwa yeye ni team Diamond, hata hivyo ameeleza katika kazi hakuna utimu.

“Kwanza ukae ukijua sijawahi kusema sifanyi kazi na mtu yeyote, Alikiba mimi ni mwanangu wa dhahabu, ni mwanangu wa gold wala wala usiseme kuna hiki na hiki japokuwa wanasema chawa, basi chawa waje vizuri kwa sababu mimi ndiye meneja wa kwanza katika muziki huu sina pingamizi kusema nitafanya kazi na mtu niogope kufanya kazi na mtu,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.

“Wote ni wanangu mimi ni mkubwa na wanae, kwa hiyo Alikiba ni mwanangu, haijawahi kuonekana hata siku moja mimi na Alikba tunagombana,” amesema Fella.

Source: TeamTz