Rapper 50 Cent amekiri kuwa ni yeye ndiye aliyevujisha episode ya 8 ya tamthilia ya POWER. Pamoja na hivyo, ratings za show hiyo zimeongezeka kwa asimilia 10 na hivyo kumfanya 50 ambaye ni mtayarishaji mkuu na muigizaji pia kusema yeye ndiye aliyefanya hivyo.
Kupitia Instagram, 50 aliandika, “POWER ratings up another 10 percent for episode 408. They glad I leaked the s— now.
50 anadaiwa kuchukua uamuzi huo baada ya episode ya show ya HBO, Game of Thrones kuleak kabla ya muda wake na ratings kwenda juu zaidi. Kituo cha Starz kinachorusha Power kilisema kitachukua hatua za kisheria dhidi ya mtu aliyevujisha episode hiyo.
Source: Dizzim online